Mafunzo haya yanahusu: Kutambua Maqam mbalimbali ya Qur'an (kama Bayati, Nahawand, Saba, Hijaz, Jiharkah, Rost, Sikah, Kurd, Ajam, Ushaq, n.k). Kuimarisha matumizi sahihi ya sauti na tajwidi. Kuunganisha sauti na maana ya Qur’an kwa ustadi wa hisia na heshima.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Katika Jitihada mbalimbali za kuimarisha ufanisi wa usomaji wa Qur’an Tukufu na kukuza vipaji vya vijana wanaojifunza Tajwidi, Mafunzo maalum ya sauti nzuri na Makam (Maqamati) ya Qur’an Tukufu yameanzishwa rasmi chini ya uongozi na usimamizi wa Ustadh Ridha Mohammad Dosa. Mafunzo haya yanalenga kutoa elimu ya kina kuhusu sayansi ya sauti (fonolojia) na namna ya kutumia (Maqamati) mbalimbali ya Qur'an ili kuufikisha ujumbe wa Qur’an Tukufu kwa ufasaha, kwa hisia na kwa uhodari wa kisanaa.
Pichani ni Mwanafunzi anayeongoza usomaji huu kama sehemu ya mazoezi na mfano hai kwa wengine:
Katika duru hizi, Mwanafunzi mahiri Talha Ramadan anaonekana akisoma sehemu mbalimbali za Qur’an Tukufu kwa kutumia makamo (Maqam) ya kitaalamu, akionyesha kwa vitendo yale anayojifunza chini ya mwalimu wake, Ustadh Ridha Mohammad Dosa.
Mafunzo haya yanahusu:
- Kutambua Maqam mbalimbali ya Qur'an (kama Bayati, Nahawand, Saba, Hijaz, Jiharkah, Rost, Sikah, Kurd, Ajam, Ushaq, n.k.)
- Kuimarisha matumizi sahihi ya sauti na tajwidi.
- Kuunganisha sauti na maana ya Qur’an kwa ustadi wa hisia na heshima.
Mafunzo haya ni ya kipekee na yamekusudiwa kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali, kutoka wanaoanza hadi wale waliopiga hatua katika fani ya usomaji wa Qur’an Tukufu.
Kwa taarifa zaidi kuhusu ratiba ya mafunzo au namna ya kushiriki, tafadhali tembelea ukurasa wetu rasmi au wasiliana moja kwa moja na uongozi wa shule kupitia namba hizi (+255657062983).
#ElimuYaQuran #MaqamatYaQuran #RidhaMohamedDosa #Tajwidi #SanaaYaUsomajiQuran
Your Comment